Over 10 years we help companies reach their financial and branding goals. Maxbizz is a values-driven consulting agency dedicated.

Gallery

Contact

+1-800-456-478-23

411 University St, Seattle

maxbizz@mail.com

Waziri wa Maji Ahimiza Huduma Bora Katika Maji Cup

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, ametumia fainali ya mashindano ya Maji Cup 2025 kufikisha ujumbe mzito kuhusu umuhimu wa huduma bora na uhakika wa maji kwa wananchi. Akiwahutubia washiriki wa mashindano hayo jijini Tanga, Waziri Aweso amesisitiza kuwa michezo hiyo ni njia ya kuhamasisha ushirikiano katika kuzuia upotevu wa maji na kuboresha mifumo ya usambazaji.

Katika fainali hiyo, Waziri Aweso aliungana na Mhe. Balozi Batilda Buriani, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kushuhudia ushindani mkali kati ya timu za ZURA (Zanzibar) na RUWASA Mwanza, ambapo ZURA ilinyakua ushindi wa bao 1–0. Katika mchezo wa netiboli, Mamlaka ya Maji Mbeya waliibuka mabingwa.

Mashindano haya yameonesha nguvu ya michezo kama nyenzo ya kuelimisha jamii na kushirikisha wadau wa maji katika uboreshaji wa huduma.